Watu wengi huingia madukani kila mara kununua computer. Huweza kuwa Desktop au laptop kulingana na mahitaji yako. Kuna baadhi ya watu huniuliza swali hili, ninataka kununua laptop, unanishauri nichukue laptop gani?
Unapohitaji kununua computer hasa laptop, kwanza kuwa makini na nini ungependa kufanya kwa kutumia laptop hiyo. Kama wewe ni mtaalamu wa masuala ya computer kwa shughuli nzito kama kudesign picha, video, beats lazima unahitaji computer yenye RAM kubwa(angalau 3GB) , video card kubwa, yenye hard disk(angalau 350GB) kubwa pia. Kwa matumizi ya nyumbani tu sio lazima iwe na RAM kubwa (2GB inatosha) au processor(1.5GHz inatosha) bali hard disk inabidi iwe na uwezo wa kutosha (Angalau 250GB).
Ewaa! Basi tusifanye mambo yawe marefu. Leo nitakutajia laptop 10, bora zaidi sokoni kwa sasa. Takwimu hizi zimekusanywa na watumiaji wengi wa computer duniani. Gharama na ubora wa laptop huenda sambamba. Lakini kumbuka kuwa kampuni iliyotengeneza laptop fulani sio lazima tu kila laptop yao inakidhi matakwa yako, zingatia Hard disk size, RAM, processor, video na graphics card, ukubwa na uzito pia ubora wa betri.

1. NANI ZAIDI YA APPLE!?
Niamini hakuna zaidi. Laptop za Apple, Macbook Air ndizo bora zaidi sokoni. Laptop hizi hutengenezwa kwa aluminium.Hutumia SSD ambazo zina kasi kama mara 4 zaidi ya Hard disk za kawaida. Zaidi Operating system yake ni safi na ya kipekee isiyoshambuliwa na virusi. Sababu kubwa ambayo huwafanya watu wasiwe na laptop hizi hasa hapa Afrika mashariki ni bei zake ghali.2. Hewlett-Packard (HP)
Ubora: 4.5/5
Watumiaji:1/5
Huweza kukaa kwa muda mrefu. Ni ngumu, ni bora, ni bei NZURI. HP ni kampuni kongwe zaidi kupita Dell na wengine. Laptop zao ndizo zinazoaminika zaidi, ni bora zaidi na bado bei zake ni nzuri zaidi. Hii ndiyo laptop bora inayotumia platform kama Windows.
3. Dell.
Ubora: 4/5Watumiaji: 3/5
Zina warranty ya muda mrefu kupita computer zote sokoni. Dell huwa na speaker zinazotoa mziki mzuri. Pia uwezo wa screen zake ni mzuri sana. Ni bora kwa matumizi ya nyumbani na ofisini. Zina nguvu kubwa sana. Computer mpya za Dell Alienware ndizo laptop zenye nguvu zaidi kupita computer zote kwa sasa.
4. Asus.
Ubora: 4/5
Watumiaji: 0.5/5
Motherboard au ramani ni muhimu kwa kifaa chochote cha elektroniki. Asus ni kampuni inayokubalika kwa kutengeneza motherboard ambazo pia hutumiwa na makampuni mengine kama Dell, Acer na Lenovo. Hivyo basi lazima wao weyewe computer zao ziwe bora kwa akili ya kawaida tu. Asus hutengeneza laptop bora. Hupata Errors chache zaidi kama unatumia platform za windows na Ubuntu.
5. Acer
Ubora: 4/5 Watumiaji: 3/5Kama unazungumzia laptop za kisasa hautaiacha acer. Kweli laptop hii ni bora na ingestahili kuwa juu kabisa katika list hii kama isingekuwa ghali kidogo. Ina nguvu kubwa ya kufanya kazi na graphics pamoja na video. Acer zilizo na touch screen zinasemekana kuwa nzuri zaidi ya laptop nyingine zenye touch screen. Betri za acer pia ni bora kwa mujibu wa maoni mbalimbali ya watumiaji wake.
Listi ya 5 zilizobaki ni kama hii hapa chini.
6. Lenovo
7. Toshiba
8. Samsung
Ni ngumu kuamini kama kweli hii ndiyo nafasi ya samsung katika kumi hizi bora zaidi. Samsung ni moja kati makampuni bora zaidi ya elektroniki duniani. Hutengeneza bidhaa nyingi na bora. Uwezekano wa idadi kubwa ya watu kutumia laptop zao uko chini kupita jinsi watu wanavyoamini simu zao. Laptop za samsung zimekuwa zikipata hitilafu mara nyingi zaidi ya hizo nyingine. Hata hivyo laptop hizi ni poa zaidi, si unajua tena, made in Seoul, China.
9. Alienware
10.Sony.
Shukrani kwa kuendelea kuwa mgeni wa Suparoja studio. Tafadhali kama kuna swali lolote lihusulo computer na teknolojia kwa ujumla usisite kuniachia swali hilo katika kipengele hapo chini ya screen kilichoandikwa NIKUFANYIE NINI? na nitakupatia majibu na ufumbuzi. Ni faraja kwangu kuweza kukusaidia pia unaweza kunipigia simu kwa namba inayopatikana katika kipengele cha about. #Asante_kwa_kuwepo.
0 maoni:
Post a Comment